Exodus 29:38-43

38 a“Kwa kawaida hiki ndicho utakachotoa juu ya madhabahu kila siku: wana-kondoo wawili wenye umri wa mwaka mmoja. 39 bUtamtoa mmoja asubuhi na huyo mwingine jioni. 40 cPamoja na mwana-kondoo wa kwanza utatoa efa moja
Efa moja ni sawa na kilo 22.
ya unga wa ngano laini uliochanganywa na robo ya hini
Robo ya hini ni sawa na lita moja.
ya mafuta yaliyokamuliwa, pamoja na robo ya hini ya divai kuwa sadaka ya kinywaji.
41 fHuyo mwana-kondoo mwingine mtoe dhabihu wakati wa machweo pamoja na sadaka za unga na za kinywaji kama vile ulivyofanya asubuhi, kuwa harufu ya kupendeza, sadaka iliyotolewa kwa Bwana kwa moto.

42 g“Kwa vizazi vijavyo itakuwa kawaida kutoa sadaka hii ya kuteketezwa kila mara kwenye ingilio la Hema la Kukutania mbele za Bwana. Hapo ndipo nitakapokutana na ninyi na kusema nanyi, 43 hHuko ndipo nitakapokutana na Waisraeli, nalo Hema la Kukutania litatakaswa na utukufu wangu.

Copyright information for SwhKC